Toleo Maalum

TFNC: Ni muhimu kuikumbusha jamii kuhusu lishe na chakula bora

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) ni mojawapo ya Taasisi ya umma inayotekeleza maju­kumu yake kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Lengo kuu la taasisi ni kud­hibiti na kutokomeza kabi­sa matatizo ya utapiamlo hapa nchini, kuhakikisha jamii inakula chakula sahihi na salama na jamii inaz­ingatia ulaji unaofaa. Taa­sisi ina majukumu ya msingi mbalimbali, miongoni mwa majukumu na wajibu wake katika jamii ni pamoja na

Toleo Maalum

ZBS inaendelea kuweka viwango bora na kusimamia ubora wa bidhaa na huduma

Taasisi ya viwango ina jukumu la kuandaa na kuvisimamia viwango na kusimamia ubora wa bidhaa zote zikiwemo za vyakula, taasisi ina­hakikisha kuwa vyakula vyote viki­wemo vinavyotengenezwa viwan­dani kama vile unga, maziwa na bidhaa zake, mafuta ya kula, mafuta yatokanayo na mimea, pia bidhaa za kilimo kama vile matunda na mboga mboga, bidhaa za oganiki, nafaka, viungo, pia vyakula vya wanyama huwekewa viwango na bidhaa hizi lazima zikaguliwe kati­ka maabara ili kuhakikisha ubora wake ndipo ziruhusiwe kwa matu­mizi ya binadamu.

Toleo Maalum

Benki ya CBA yataja faida nyingi za Mfumo wa Bulk Mobile Payment

Bulk Mobile Payment ni mfumo unaowawezesha wateja kufanya malipo ya mtu mmoja mmoja au ya watu wengi kwa wamiliki wa simu wenye huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya mtandao. Hii inahusisha waajiri wanaofanya malipo kwa wafanyakazi ambao hawapo katika mfumo rasmi wa ajira (vibarua), makampuni ya bima yanayofanya malipo kwa wateja wao wasio na akaunti za benki, utoaji wa mikopo kwa wateja wasio na akaunti za benki, makampuni ya usafirishaji yanayotoa posho na mishahara kwa wasafirishaji (madereva) nk.

Toleo Maalum

Juhudi za Shirika la Plan International katika kuboresha sekta ya elimu nchini

Miongoni mwa mafanikio katika elimu ni pamoja na kuongezeka kwa uandikishwaji wa watoto kwenye elimu ya Awali, Msingi na Sekondari. Kwa mujibu wa Kitabu cha Takwimu za Elimu cha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaani Basic Education Statistics in Tazania, (BEST 2017), uandikishwaji halisi (net enrolment) kwa elimu ya Awali mwaka 2017 ulikuwa ni 1,517,670 kutoka 639,080 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la 237%.Hata hivyo, uandikishwaji halisi kwa ngazi hii ulishuka kwa 2.9% kutoka wanafunzi 1,562,770 mwaka 2016 hadi 1,517,670 mwaka 2017.

Toleo Maalum

UCHAMBUZI BAJETI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019 NA 2019/2020

Katika mwaka wa Fedha wa 2018/2019, Wizara ya Nishati ilikadiria kukusanya na kutumia Shilingi 1.69 Trilioni, katika makadirio hayo, shilingi 1. 665 trilioni zilitengwa kwa ajili ya Maendeleo na Shilingi 27,145,014,000 zikiwa ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Hadi kufikia Disemba 2018, kiasi cha shilingi bilioni 275.40 zilikuwa zimepokelewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo, hivyohivyo, Shilingi bilioni 12.1 zikiwa zimepokelewa kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Toleo Maalum

Uchambuzi wa HakiRasilimali kuhusu bajeti ya Wizara ya madini na Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2018/19 na 2019/2020

Sekta ya uziduaji (Mafuta, Madini na gesi asilia) ni eneo muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla, takwimu zinaonesha kuwa sekta ya uziduaji nchini inakadiriwa kuchangia takribani asilimia 5 (2018) ya pato la Taifa ambapo, Dira ya Taifa ya maendeleo inakadiria kwamba hadi kufikia Mwaka 2025 mchango wa sekta ya madini unatarajiwa kuongezeka hadi kufikia asilimia 10 ya pato zima la Taifa.

TEST

Mwananchi