In Summary

Yanga ambayo imepangwa kundi D pamoja na timu za Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda pamoja na USM Alger ya Algeria wameshindwa kutamba katika mechi zao zote mbili walizocheza.

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi klabu ya  Yanga, imeendelea kushika mkia kwenye kundi lao wakiwa na pointi moja tu.

Yanga ambayo imepangwa kundi D pamoja na timu za Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda pamoja na USM Alger ya Algeria wameshindwa kutamba katika mechi zao zote mbili walizocheza.

Katika mechi hizo Yanga imefungwa ugenini na USM Alger mabao 4-0, pia ikatoa suluhu kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Taifa dhidi ya Rayon.

Kwa matokeo hayo, USM Alger ndiyo vinara ambao wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi 4, Gor Mahia na Rayon Sports wanafuata wote wakiwa na pointi 2 kila mmoja na Yanga inayonolewa na kocha Mcongo Mwinyi Zahera ndiyo wa mwisho na pointi hiyo moja.