In Summary
  • Wenger aliongoza mechi ya mwisho ya Arsenal  Jumapili iliyopita dhidi ya Huddersfield kwenye Uwanja wa John Smith huku kikosi chake kikiibuka na ushindi kwa bao 1-0.

Mkutano wake wa mwisho na vyombo vya habari, Kocha Arsene Wenger alisema wachezaji kutoka Afrika walikuwa na mchango mkubwa katika taaluma yake akiwa meneja wa klabu ya Arsenal nchini Uingereza.

Wenger aliongoza mechi ya mwisho ya Arsenal  Jumapili iliyopita dhidi ya Huddersfield kwenye Uwanja wa John Smith huku kikosi chake kikiibuka na ushindi kwa bao 1-0.

Wenger anaondoka Arsenal baada ya kuongoza mechi 1,235 na kushinda mechi 716 huku akiwa na akiba ya mabao 2,298. Hata hivyo hadi sasa Arsenal bado haijamteua mrithi wake licha ya kuwapo tetesi kuhusu makocha ambao huenda wakachukua mikoba yake.

Kuanzia Rais wa sasa wa Liberia George Weah huko Monaco hadi mchezaji wa mwisho aliyesaini raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, Wenger ametambua mchango muhumu wa wachezaji hao kutoka Afrika.

Kuwasajili na kuwakuza kisoka wachezaji bora zaidi wa Afrika ni kitu ambacho Wenger amekifanya katika miaka yake yote 22 amekuwa na Arsenal.

Sababu ya hili kutokuwa jambo la kushagaza, ni kuwa wachezaji 16 kutoka Afrika waliichezea Arsenal chini ya usimamizi wake Wenger.

 

Jeshi la Wenger kutoka Afrika:

Emmanuel Adebayor (Togo)

Alex Iwobi (Nigeria)

Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon)

Nwankwo Kanu (Nigeria)

Marouane Chamakh (Morocco)

Lauren (Cameroon)

Kaba Diawara (Guinea)

Quincy (Ghana)

Emmanuel Eboue (Ivory Coast)

Alex Song (Cameroon)

Mohamed Elneny (Misri)

Kolo Toure (Ivory Coast)

Emmanuel Frimpong (Ghana)

Armand Traore (Senegal)

Gervinho (Ivory Coast)

Christopher Wreh (Liberia)

 

1. Nwankwo Kanu

Mshindi mara mbili wa tuzo la mchezaji bora Afrika, Nwankwo Kanu ni mmoja wachezaji bora zaidi kutoka Afrika kuwai kufanya kazi chini wa Arsene Wenger huko Arsenal.

Akiwa na Arsenal Mnigeria huyo alishinda vikombe viwili vya Premier League na FA na pia Kombe la Ngao ya Jamii.

Baada ya kujiunga na Arsenal mwaka 1999 Kanu alifunga magoli 44 kwenye mechi 198 alizocheza kabla ya kuhamia West Bromwich Albion mwaka 2004.

Anakumbukwa sana kwa ‘hat-trick’ yake ya pili dhidi ya Chelsea.

2. Lauren

Raia wa Cameroon Lauren alifunga mabao 9 kwa mechi 241 katika mechi alizocheza, lakini kawaida alikuwa ni mchezaji aliyekuwa anategemewa zaidi. Alisajiliwa na Wenger mwaka 2000 kama Wing'a na kuibuka kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi katika safu ya ulinzi Ligi Kuu England na baadaye  alihamia Portsmouth mwaka 2007.

Hivyo Lauren alishinda vikombe vingi zaidi akiwa na Asenal chini ya Arsene Wenger.

3. Kolo Toure

Kolo Toure alikumbwa na matatizo nyakati za mwisho mwisho akiwa na Arsenal. Alisajiliwa na Wenger kwa Paunia 150,000. Beki hiyo raia wa Ivory Coast ambaye pia alicheza kama mshambuliaji, alikuwa mmoja wa wale waliotegemewa kwenye ligi hiyo yenye ushindani.

Toure alicheza na magwiji wengine kama Sol Campbell, William Gallas na pia Philip Senderos.

Alishinda mataji matano akiwa na Gunners na kuchangia mabao 14 kwa jumla ya mechi 326 alizocheza.

4. Alex Song

Alex Song alikuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa Afrika waliosajiliwa mikononi mwa Wenger.

Licha ya Song kutofikia kiwango cha watangulizi wake kama Patrick Viera na Gilberto Silva,  lakini alitoa mchango mkubwa kwa Arsenal.

Alikuwa ni mchezaji mzuri na hata baada ya kuhamia Portsmouth, aliamua kulekea huko Barcelona. Hata hivyo hakushinda taji lolote akiwa na Arsenal.

Alisakata kambumbu ya hali ya juu kwenye mechi 218 akiwa na Wenger.

5. Emmanuel Adebayor

Yawezekana Emmanuel Adebayor alimuita Wenger mtu feki, lakini bado anastahili kumshukuru kwa kumkuza tangu alipomsajili kutoka Monaco mwaka 2006.

Adebayor haukuweza kuichezea Arsenal kwa misimu mitatu lakini ni mmoja wa wachezaji bora zaidi kuichezea Arsenal wakati wa kipindi cha Wenger.

Raia huyo wa Togo alicheza jumla ya mechi 143 na kufunga mabao 62.