In Summary
  • Man City imefanikiwa kutwaa ubingwa wiki hii baada ya majirani zao Man United kufungwa na West Bromwich

London, England. Pep Guardiola anatarajiwa kutia saini mkataba mpya na klabu ya Manchester City.

Guardiola anatarajiwa kupata bonasi ya Pauni10 milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Kocha huyo mwenye miaka 47, anatarajiwa kubaki Man City hadi mwaka 2020 baada ya kupata mafanikio katika msimu wake wa pili.

Guardiola amewavutia wamiliki wa klabu hiyo kutoka Abu Dhabi, baada ya kuipa Man City ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu ikiwa na mechi mkononi.

Kocha huyo anatarajiwa kuvuna Pauni15 milioni kwa mwaka atakapotia saini mkataba huo.

Mbali na Guardiola, Man City inatarajiwa kuwabakiza baadhi ya nyota wake waliotamba msimu huu akiwemo kiungo mshambuliaji Kevin De Bruyne.