In Summary
  • Ole Gunnar Solskjaer amesema hashangai kocha wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino kuhuishwa na mpango wa kujiunga na Manchester United.

London, England. Ole Gunnar Solskjaer amesema Kocha wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino ana sifa za kuinoa Manchester United.

Solskjaer alisema Pochettino ni kocha bora anayestahili kujaza nafasi ya Jose Mourinho aliyetimuliwa baada ya kuboronga katika mashindano ya msimu huu.

Nguli huyo wa zamani wa timu hiyo, alisema Pochettino amefanya kazi nzuri Spurs na hashangai kuhusishwa na mpango wa kutua Old Trafford.

Kauli ya kocha huyo wa muda, ametoa kauli hiyo wakati Man United ikiajiandaa kwa mchezo dhidi ya Spurs ambao utachezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Wembley, London.

Licha ya kushinda mechi tano mfululizo, Solskjaer alisema Spurs ni timu bora inayocheza soka kwa kiwango bora.

“Anafanya kazi nzuri. Sishangai kuhusishwa na mpango wa kujiunga na Manchester United, lakini siyo kazi yangu kupima uwezo wa makocha,” alisema Solskjaer.

Man United imerejea London ikitokea katika ziara fupi ya mapumziko mjini Dudai walipokwenda kujiandaa kwa mechi dhidi ya Spurs.