In Summary
  • Mshambuliaji nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo amevamiwa na shabiki uwanjani wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Italia.

Rome, Italia. Cristiano Ronaldo amevamiwa na shabiki uwanjani katika mchezo ambao Juventus ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Sassuolo.

Shabiki huyo alimvamia mchezaji huyo baada ya kuvamia uwanja na kwenda kumkumbatia wakati mchezo huo ukiendelea.

Tukio hilo lilitokea kipindi cha pili, baada ya shabiki huyo kuonyesha furaha yake kutokana na kiwango bora cha Juventus.

Ronaldo alifunga bao moja katika mchezo na mengine yalifungwa na Sami Khedira na Emre Can.

Ronaldo aliyejiunga na Juventus akitokea Real Madrid katika usajili wa majira ya kiangazi msimu uliopita, amefunga mabao 20.