In Summary
  • Wayne Rooney ana kibarua kigumu ya kunusuru ndoa yake kwa mara nyingine, baada ya kubambwa akiwa na mwanamke muuza baa

Florida, Marekani. Ndoa ya nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya England, Wayne Rooney na mkewe Coleen ipo shakani.

Rooney anadaiwa kunywa pombe kwa saa 10 akiwa na muuza baa Vicki Rosiek katika mji wa Florida, Jumapili ya wiki iliyopita.

Nguli huyo anayecheza klabu ya DC United, aliponda raha na mrembo huyo hadi saa 8:30 usiku kitendo ambacho kilimkera Coleen.

“Umenidhalilisha tena, Coleen hakuwa na hasira ingawa alionekana akiwa amechukizwa na kitendo cha Wayne,” kilisema chanzo ndani ya familia hiyo.

Coleen anadaiwa alipanda ndege kurejea England. Tukio limetokea wiki kadhaa baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United kukutwa akiwa amelewa Uwanja wa Ndege wa Washington DC.