In Summary
  • Washambuliaji hao wawili kila mmoja ametwaa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka mara tano

Madrid, Hispania. Tangu Februari 10, Real Madrid ilipoichakaza Real Sociedad kwa mabao matatu ‘hat-trick’ Cristiano Ronaldo.

Mshambuliaji huyo amekuwa na rekodi ya kuvutia akiwa amefunga katika kila mchezo aliokuwa uwanjani akicheza katika mechi 11 amefunga mabao 21.

Mafanikio hayo yamefikiwa na mchezaji mmoja ambaye ni kinara wa ufungaji wa muda wote wa Real Madrid akiwa na mabao 448.

Kutokana na hali hiyo, Cristiano amekuwa na mchango wa kipekee katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa.

Alifunga dhidi ya Paris Saint-Germain katika raundi 16 bora na dhidi ya Juventus katika robo fainali, amefunga mabao sita katika kipindi hicho.

Katika mechi ya mwisho dhidi ya Wataliano hao alifunga bao lililozua utata baada ya kupata penalti katika dakika za nyongeza na kuisaidia timu yake kufuzu kwa nusu fainali.

Mshambuliaji huyo wa Madrid amekuwa ni mtaalamu wa kufunga katika mechi za mashindano ya Ulaya ukiwa chini ya kiwango anakufungashia virago.

Mchezaji pekee anayemkaribia kati miaka hii kumi, Leo Messi anayekula naye sahani moja Ronaldo katika hatua ya makundi wawili hao kila mmoja amefunga mabao 60, lakini katika hatua ya mtoano mambo ni tofauti.

Ronaldo amekuwa bora katika robo fainali

Katika hatua 16 bora, Leo ameongoza kwa kufunga mabao 24 dhidi ya 20, lakini kuanzia hapo, Cristiano amekuwa bora zaidi ya Muargentina huyo. Kwa mfano katika robo fainali iliyomalizika wiki hii. Wakati Leo na timu yake wakitolewa naye akiondoka patupu, Ronaldo amefanikiwa kufunga mabao matatu na kuiondoa Juventus.

Kwa ujuma tofauti kati ya nyota hao katika kufunga mabao katika hatua ya mtoano ni 23 kwa 10, Mreno huyo akiongoza kwa kufunga tangu alipotua Real Madrid mwaka 2009.

Kwa ujumla Ronaldo amekuwa na rekodi ya kutisha katika Ligi ya Mabingwa akiwa amefunga mabao 120 hadi sasa.