In Summary

Inadaiwa Arsenal ipo tayari kuachana na beki huyo katika dirisha kubwa lijalo la majira ya joto endapo kuna timu itafika dau la Euro 50 milioni,

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez inadaiwa anataka kumnasa beki wa kulia wa Arsenal, Hector Bellerin, kwa ajili ya kumpa changamoto Dani Carvajal ambaye hana mpinzani katika nafasi hiyo.

Inadaiwa Arsenal ipo tayari kuachana na beki huyo katika dirisha kubwa lijalo la majira ya joto endapo kuna timu itafika dau la Euro 50 milioni, lakini Madrid pia inaweza kukumbana na upinzani kutoka Juventus.