In Summary

Straika wa Simba Emmanuel Okwi hakuwepo katika kikosi cha timu kilichocheza mechi ya Kimataifa dhidi ya JS Saoura, Straika wa Simba Emmanuel Okwi hakuwa katika kikosi cha timu hiyo kilichocheza dhidi ya JS Saoura.

Kikosi cha Simba kilicheza mechi ya ugenini katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ua JSS na kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0. Kikosi hicho mbali ya kufungwa kulikosa huduma ya mshambuliaji wake Emmanuel Okwi ambaye aliachwa kutokana na kuwa mgonjwa.

 Wiki hii kulikuwa na taarifa za mitandaoni kuwa Okwi ameondoka na kwenda kwao Uganda.

 Katika mazoezi ya kujindaa na mechi ya AS Vita ambayo Simba watacheza Jumamosi uwanja wa Taifa Okwi alionekana akiwa anafanya mazoezi ya pamoja na wenzake.

 Kikosi hiko cha Simba kilifanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veterans leo kuanzia saa 10:00 jioni.