In Summary
  • Simba inaenda kucheza na Al Masry, wakati Yanga inaenda kucheza na Township Rollers ya Botswana, jambo ambalo Okwi anasema kwa mechi walizocheza nyumbani ziwafunze kujua wapinzani wao wana mbinu gani. 

STAA wa Simba, Emmanuel Okwi amesema timu za Tanzania, zinazowakilisha kwenye michuano ya kimataifa, zina nafasi ya kufanya maajabu, kikubwa ni kuzingatia nidhamu ya mchezo wawapo uwanjani.

Simba inaenda kucheza na Al Masry, wakati Yanga inaenda kucheza na Township Rollers ya Botswana, jambo ambalo Okwi anasema kwa mechi walizocheza nyumbani ziwafunze kujua wapinzani wao wana mbinu gani. 

"Inawezekana tukashinda ugenini, tujipange na kujua tunaenda kufanya nini, akili zetu zitulie kwa ajili ya majukumu hayo,"

"Mfano mzuri Al Masry wana mbinu nyingi kuanzia wachezaji wenyewe wanapokuwa uwanjani,wanajua namna ya kuwatoa mchezoni wapinzani,nadhani tumewasoma kwa sehemu,hilo litupe alama ya umakini,"anasema.

"Hata mashabiki wao ni wale ambao wanapenda kutisha wapinzani na kumfanya mchezaji atoke mchezoni,tukivumudu hivyo,tutaonyesha kitu kitakachowastajabisha na hawataamini,"anasema.