In Summary
  • Timu hizo zimekuwa na utamaduni wakuuzina wachezaji

Madrid, Hispania.Real Madrid na Bayern Munich wamekutana mara nyingi zaidi katika historia ya mashindano hayo, lakini jambo la kuvutia ni wachezaji saba tu ndiyo wamechezea timu zote mbili.

Wachezaji watatu kati ya saba watacheza katika nusu fainali itakayopigwa baadaye mwezi huu, wakati wanne waliobaki wakiwa wameondoka katika klabu hizo.

Hapa chini na wachezaji saba waliopita katika klabu hizo.

Paul Breitner

Mjerumani huyo aliihama Real Madrid akitokea Bayern baada ya kutwaa Kombe la Dunia 1974.

Ze Roberto

Mbrazili huyo alikuwa katika kikosi cha Real Madrid kilichotwaa taji la saba la Ligi ya Mabingwa.

Arjen Robben

Ni mchezaji wa kikosi cha sasa cha Bayern, lakini alishakaa kwa misimu miwili Real Madrid.

Hamit Altntop

Alikuwa na miaka mitano yenye mafanikio Bayern, lakini alishindwa kutamba katika kikosi cha Real.

Toni Kroos

Ni Mjerumani ambaye yupo katika kikosi cha sasa cha Real Madrid aliyesajiliwa akitokea Bayern.

Xabi Alonso

Baada ya mafanikio yake ya miaka mitano Madrid, alimalizia soka lake Bavaria.

James Rodriguez

Kiungo wa Bayern anayecheza kwa mkopo akitokea Real Madrid.