In Summary
  • Neymar alijitokeza kwa mara ya kwanza katika tamasha la amfAR, akiwa anatembelea fimbo mbili, huku mguu wake wa kulia ukiwa umefungwa plasta ngumu ikiwa na kiatu maalum.

Nyota wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar ametokeza hadharani kwa mara ya kwanza tangu aumie mguu wa kulia.
Neymar alijitokeza kwa mara ya kwanza katika tamasha la amfAR, akiwa anatembelea fimbo mbili, huku mguu wake wa kulia ukiwa umefungwa plasta ngumu ikiwa na kiatu maalum.
Akiwa amevalia suti nyeusi, Neymar aliambatana na mpenzi wake, Bruna Marquezine na kupiga picha ya pamoja katika zuria jekundu na baadaye kupigana busu kabla ya kuondoka.
Neymar ambaye alivunjika mfupa wa mguu wake wa kulia Februari 25, aliwaambia waandishi wa habari wa Brazil kuwa amebakiza mwezi mmoja kabla ya kurejea uwanjani na hivyo ana matumaini ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Dunia nchini Russia.