In Summary

Endapo watafanikiwa kutwaa ubingwa Aprili, Man City itaweka rekodi ya kutwaa mapema zaidi taji hilo

Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany sasa anajiandaa kukabidhiwa ubingwa wa Ligi Kuu na watani zake wa jadi Manchester United.

Manchester City sasa wanahitaji kushinda mechi zao mbili tu ili kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu England.

Kiungo David Silva alifunga mabao mawili na kukifanya kikosi cha Pep Guardiola kuongoza kwa tofauti ya pointi 16.

Kama Man City wataifunga Everton ugenini Machi 31, na baadaye watawakaribisha watani zao Man United kwenye Uwanja wa Etihad hapo Aprili 7, endapo watashinda basi watakuwa mabingwa.

Nahodha wa Citym Kompany alisema: “Kila moja aliyekatika upande wa blue katika jiji la Manchester anajua inatokea mara moja tu maisha kutwaa ubingwa kwa kuifunga Man United.

“Lakini, kwa bahati mbaya hawatatukabidhi kirahisi sisi.

“Kila ushindi unatuweka karibu na kutimiza lengo letu, lakini tunataka kubaki katika hali hii hadi mwisho wa msimu na kiwezekana na msimu ujao pia.”

City ilipata bao la kuongoza dakika ya 10, wakati Gabriel Jesus alipopitisha mpira kwa Raheem Sterling, aliyepitisha krosi kwa Silva aliyemalizia mpira wavuni.

Mhispania huyo Silva alifunga bao la pili dakika ya  50, akipokea pasi ya Fernandinho na kupiga shuti la juu lililomwacha kipa wa Stoke City, Butland asijue la kufanya.