In Summary

Taarifa za awali zikidai City ilikuwa inaongoza mbio hizo

KLABU ya Shakhtar Donetsk imethibitisha kwamba kiungo wao, Fred, atakwenda katika klabu moja ya Manchester katika dirisha kubwa lijalo la majira ya joto na hii inathibitisha kwamba klabu moja kati ya Man City au Man United itamchukua.

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Sergei Palkin, amethibitisha kwamba kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil ataondoka Juni mwaka huu na dau lake linakadiriwa kufikia Pauni 50 milioni huku taarifa za awali zikidai City ilikuwa inaongoza mbio hizo.