In Summary
  • Thierry Henry mmoja wa washambuliaji mahiri kuwahi kuitumikia Arsenal, kwa sasa ni Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Ubelgiji na yupo katika orodha ya makocha wanaowaniwa kuinoa timu ya Daraja la kwanza ya Aston Villa ambayio imemtimua kazi Kocha Steven Bruce.
  • Henry anatarajiwa kuchuana vikali na mlinzi na nahodha wa zamani wa Chelsea na England, John Terry ambaye aliitumikia timu hiyo kabla ya kutundika daluga.

London, England. Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa ni Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Ubelgiji, Thierry Henry, inasemekana anafukuzia kibarua cha kuinoa Aston Villa.

Henry atachuana na nahodha wa zamani wa Chelsea na England, John Terry ambaye aliitumikia timu hiyo kabla ya kustaafu na ndiye anayepigiwa chapuo zaidi la kuchukua nafasi ya Steven Bruce aliyetimuliwa.

Bruce ametimuliwa juzi kutokana na matokeo mabaya ya tuimu hiyo katika Ligi Daraja la Kwanza, ambapo hadi sasa ipo nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi 11 ikishinda tatu sare sita na kupoteza miwili.

Mmiliki mpya wa klabu hiyo, bilionea kutoka Misri, Nassef Sawiris, ameweka wazi sababu za kumtimua Bruce akisema kushindwa kuipa mafanikio kama alivyoahidi.

Sawiris alisema amefadhaishwa na mwenendo wa timu ambayo nia yake ni kuhakikisha inarejea Ligi Kuu England na kuwa moja ya timu shindani, hivyo anataka Kocha atakayeipa mafanikio.