In Summary
  • Sasa hakuna kificho, kuanzia msimu ujao wa 2018/19, mshindi huyo wa tuzo tano za Ballon D'or atavaa jezi nyeupe na nyeusi na sio nyeupe iliyozoeleka. Taarifa za Ronaldo kuhamia Italia zilianza kuzagaa majumaa kadhaa iliyopita.

NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo sasa ni mali klabu ya Juventus ya Italia. Habari ndio hiyo. Ni kwamba, Ronaldo amesaini mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa kihistoria wa Series A.

Sasa hakuna kificho, kuanzia msimu ujao wa 2018/19, mshindi huyo wa tuzo tano za Ballon D'or atavaa jezi nyeupe na nyeusi na sio nyeupe iliyozoeleka. Taarifa za Ronaldo kuhamia Italia zilianza kuzagaa majumaa kadhaa iliyopita.

Taarifa hizo zinasema kuwa Ronaldo amesaini mkataba wa miaka minne kuitumikia bibi kizee cha Torino, wenye thamani ya Pauni milioni 105. Tetesi hizo zilitiwa nguvu na kikao kati ya wakala wa mreno huyo, Jorge Mendes na Rais wa Real Madrid, Fiorentino Perez.

Mazungumzo kati ya Juventus na Real Madrid yakaanza rasmi. Baada ya kung'olewa na timu take ya ureno kwenye michuano ya Kombe la Dunia, duru za kuaminika zikasema Ronaldo ameonekana Italia.

Sababu za kuondoka kwa Ronaldo, mwenye umri wa miaka 31, pale Santiago Bernabeu, zinadaiwa kuwa ni kutoafikiana na Perez kuhusu mkataba ambapo Ronaldo alitaka mkataba wake uboreshwe, huku sababu nyingine ikiwa ni tetesi za ujio wa Neymar.

Itakumbukwa kwamba, mara baada ya kuiongoza Los Blancoz kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya mara tatu mfululizo, Ronaldo alinukuliwa akisema kuwa, taji hilo ndio LA mwisho kuishindia Real Madrid huku akiwashukuru mashabiko licha ya baadae kuzikana.