In Summary
  • Alisema Senderos aliyekaa Arsenal miaka saba na kutwaa taji la FA na Ngao ya Jamii ambaye kwa sasa anacheza soka nchini Marekani kwenye klabu ya Houston Dynamo alikuwa anakosa utulivu kabla ya mechi inayohusisha washambuliaji wenye mbio na nguvu.

London, England, mlinzi wa zamani wa Arsenal, Chelsea na timu ya Taifa ya Ufaransa, William Gallas amefichua kuwa aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Arsenal enzi hizo, Philippe Senderos alikuwa akipandwa na presha kabla ya mechi kwa kumuhofia Didier Drogba.

Alisema Senderos aliyekaa Arsenal miaka saba na kutwaa taji la FA na Ngao ya Jamii ambaye kwa sasa anacheza soka nchini Marekani kwenye klabu ya Houston Dynamo alikuwa anakosa utulivu kabla ya mechi inayohusisha washambuliaji wenye mbio na nguvu.

Alisema Gallas raia wa Ufaransa ambaye alikuwa London kwa ajili ya kushiriki michezo ya kuwachangia watu wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa, alisema alikuwa na jukumu la kumtuliza Senderos.

“Kocha wa Arsenal wakati huo Arsene Wenger', aliwahi kunipa kazi ya kumtuliza Senderos kabla ya mechi ngumu hasa dhidi ya Chelsea kwa sababu alikuwa anamuogopa sana Drogba muda wote anakuwa na hofu,” alisema.

Gallas mwenye miaka 41 kwa sasa alisema kuwa Senderos alikua hapati presha wanapocheza na timu kama Barcelona licha ya kusheheni vipaji lakini inapotokea mechi dhidi ya Chelsea alikua akianza kuwahimiza kusaidiana kumkaba Drogba tangu asubuhi ya siku ya mechi.

Alisema kuwa amebaini tatizo la hofu halikuwa likimsumbua Senderos pekee nali hadi sasa kuna wachezaji wengi wa Arsenal ambao huingia mchezoni wakiwa tayari wamekubali kufungwa.