In Summary
  • Katika dirisha dogo lililopita, Everton ilimnasa winga Theo Walcott kwa dau la Pauni 25 milioni, lakini sasa imenogewa na inamtaka Wilshere.

EVERTON imerudi tena katika kambi ya Arsenal na imemfungia kazi kiungo, Jack Wilshere, ambaye anaweza kupatikana bure mwishoni mwa msimu kwani  mkataba wake utakuwa umemalizika.

Katika dirisha dogo lililopita, Everton ilimnasa winga Theo Walcott kwa dau la Pauni 25 milioni, lakini sasa imenogewa na inamtaka Wilshere ambaye hivi karibuni alikiri bado hana mpango wa kusaini mkataba mpya Emirates.

Wilshere amerudi vizuri katika kikosi cha Arsenal baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu na ingawa kocha, Arsene Wenger anataka abakie klabuni hapo, lakini hatima ya staa huyo bado imebaki hewani.