In Summary

Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Angelique Kerber, kucheza tangu atwae ubingwa wa Wimbledon akifungwa kwa 6-4 6-1 na kufungwa kirahisi.

Montreal, Canada. Bingwa wa michuano ya Wimbledon kwa wanawake Angelique Kerber, ameyaaga mashindano ya mwaka huu ya Rogers Cup baada ya kufungwa na Alize Cornet kutoka Ufaransa.

Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Angelique Kerber, kucheza tangu atwae ubingwa wa Wimbledon akifungwa kwa 6-4 6-1 na kufungwa kirahisi.

Naye Maria Sharapova akicheza huku mvua kubwa ikinyesha mjini Montreal, alipata ushindi wake wa 25 dhidi ya mchezaji mwenzake kutoka Russia, Daria Kasatkina kwa seti mbili za 6-0, 6-2.

Alize Cornet, mchezaji ambaye hajawahi kushika nafasi ndani ya 10 bora katika viwango vya ubora, atacheza na mchezaji kutoka Australia, Ashleigh Barty.

Maria Sharapova bingwa mara tatu wa Grand Slam mwenye miaka 31, alihitaji saa 1:16 kufikia ushindi kiasi kwamba Kasatkina.

Mchezo uliosubiriwa kwa hamu sana ni ule wa jana usiku uliowakutanisha Mwingereza, Johanna Konta dhidi ya nyota wa Belarus, Victoria Azarenka.