In Summary
  • Barcelona imetangaza dau la kumsajili mchezaji nyota wa Chelsea Willian katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwaka huu.

Madrid, Hispania. Barcelona imeongeza kasi ya kumsajili winga wa Chelsea Willian, baada ya kutenga Pauni50 milioni.

Barcelona imetangaza mpango wa kumngoa nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, licha ya kuibuka tetesi za kumtaka Neymar.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Hispania, wamedai watakuwa tayari kutoa fedha na mchezaji ili kupata saini ya Willian ambaye awali aliwahi kuhusishwa na mpango wa kutua Manchester United.

Barcelona imesema itamtoa Malcom ambaye amekosa namba katika kikosi cha kwanza licha ya kununuliwa kwa Pauni38 milioni majira ya kiangazi msimu uliopita akitokea Bordeaux.

Hii ni mara ya tatu Barcelona kutaka saini ya Willian (21) ambaye amekuwa chaguo la kwanza kwa kocha Maurizio Sarri.

Klabu ya Dalian Yifang inayoshiriki Ligi Kuu China imewahi kuweka bayana kuwa inamtaka winga huyo kwenda kuimarisha kikosi chake.

Chelsea iliwahi kukataa ofa ya Pauni65 milioni ilizotolewa kwa ajili ya kumpiba bei mchezaji huyo. Nyota huyo amebakiza miezi 18 kabla ya mkataba wake kumalizika.

Wakati huo huo, Barcelona jana ilichezea kichapo baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Levante katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Mfalme.