In Summary
  • Kiungo huyo alikuwa anakaribia kujiunga na Shaktar Donetsk katika dirisha la Januari, lakini uhamisho huo ulikwama.

ARSENAL imeanza kumfukuzia kinda wa Kibrazili, Maycon, anayekipiga katika klabu ya Corinthians ya Brazil na inadaiwa kuwa klabu yake ipo tayari kuachana naye kwa dau la Pauni 9 milioni tu.

Kiungo huyo alikuwa anakaribia kujiunga na Shaktar Donetsk katika dirisha la Januari, lakini uhamisho huo ulikwama na sasa Arsenal imekuwa mstari wa mbele katika mbio za kumsaka katika dirisha kubwa la majira ya joto.