In Summary
  • Biashara katika mechi zao za nyumbani msimu huu, imefungwa na Mwadui, Simba pamoja na Alliance huku mchezo wao wa hivi karibuni waliaadhibu Yanga kwa bao 1-0 kwenye uwanja huo.
  • Biashara United wamepoteza mchezo huo na kujiweka kwenye hatari ya kucheza play off.

Timu ya Alliance FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Karume, Musoma  mkoani Mara leo Jumatano.

Ushindi huo umewafanya Alliance kufikisha pointi 44 kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakiwa wamecheza michezo 36 huku Biashara wana alama pointi 40 katika michezo 35.

Mchezo huo pia ulikuwa ukiahirishwa mara kwa mara kwa hiyo kucheza kwao leo kumekata hamu ya mashabiki wa Musoma ambao walikuwa wanasubilia kwa hamu mechi hiyo.

Biashara katika mechi zao za nyumbani msimu huu, imefungwa na Mwadui, Simba pamoja na Alliance huku mchezo wao wa hivi karibuni waliaadhibu Yanga kwa bao 1-0 kwenye uwanja huo.

Mechi nyingine iliyopigwa leo, Mbeya City 1- 0 Coastal Union.