In Summary

Three Lions Wameishangaza Dunia kwelikweli. Wengi wamekuwa wakijiuliza imekuwaje wakaweza kutafuna mfupa uliowashinda Argentina na Lionel Messi wao, Brazil na Neymar wao, Ureno na bishoo wao, Cristiano Ronaldo.

Moscow, Russia. Wameweka rekodi ya kutinga nusu fainali baada ya miaka 28, ikiwa ni mara ya tatu katika historia ya taifa lao. wana matumaini ya kubeba ndoo, tangu wafanye hivyo mwaka 1966. Ni kwamba, wamekuja Russia, wakiwa na nia ya kubeba ndoo.

Three Lions Wameishangaza Dunia kwelikweli. Wengi wamekuwa wakijiuliza imekuwaje wakaweza kutafuna mfupa uliowashinda Argentina na Lionel Messi wao, Brazil na Neymar wao, Ureno na bishoo wao, Cristiano Ronaldo.

Kumbe Three Lions wana siri kubwa aisee. Ndio wajukuu wa Malkia walitinga hatua ya 16 bora kwa mipango. Wakavuka hadi robo fainali kwa mipango. Sasa wametinga nusu fainali kwa mipango hiyo hiyo. Kama huamini msikilize Kyle Walker.

Akizungumza na kituo kimoja cha habari, katika kambi yao huko urusi, ikiwa ni takribani masaa 24, kabla ya kuwavaa Croatia kwenye mechi ya pili ya nusu fainali, itakayopigwa kesho, beki wa Tottenham Kyle Walker, amefichua kuwa, kilichowabeba ni undugu. Huamini? Kumbe hao jamaa wanaishi kama ndugu huko Russia.

 

 

Walker anasema, wakati Gareth Southgate, alipotangaza kikosi chake, kila mtu alimshangaa. Kikosi chenye watu kama Harry Maguire, ilikuwa ni ngumu kuwapa nafasi hata ya kuvuka hatua ya makundi, na kwa kutambua hilo waliamua kuishi kwa mshikamano mkubwa ndani na nje. Moyo wao waliulekeza katika kuisaidia timu.

"Sikiliza, haijalishi ni wapi ulipotoka, mle ndani tunaunganishwa na kitu kimoja, Bendera yetu. Tunaishi kama ndugu, tunajichukulia kama watoto wa baba mmoja, sote ni wajukuu wa Malkia, hakuna ubaguzi, hakuna kujiona bora, moyo wetu ni mmoja. Hii ndio siri yetu, hii ndio nguvu yetu," alisema Walker.