In Summary
  • Maelfu ya mashabiki walijitokea kuilaki timu yao iliyorejea nyumbani baada ya kuondolewa na Ubelgiji katika robo fainali ya Kombe la Dunia linaloendelea nchini Russia.

Rio de Janeiro, Brazil. Nahodha wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar, amethibisha hasira zake kwa mashabiki baada ya kuwakimbia kwenye uwanja wa ndege mjini Rio de Janeiro.
Maelfu ya mashabiki walijitokea kuilaki timu yao iliyorejea nyumbani baada ya kuondolewa na Ubelgiji katika robo fainali ya Kombe la Dunia linaloendelea nchini Russia.
Msafara wa Brazil, ulirejea mjini Rio de Janeiro, Jumapili huku kiu ya mashabiki wengi ikiwa ni kumuona nahodha wao Neymar ambaye anakipiga Paris Saint Germany (PSG) ya Ufaransa.
Hata hivyo mashabiki hao walipigwa na butwaa baada ya kushindwa kumuona Neymar hata baada ya msafara wote kutoka nje ya uwanja na kuanza kuingia kwenye gari tayari kuondoka uwanjani hapo.