In Summary

Tangu kuanza kwa msimu huu Pogba na Mourinho wamekuwa hawana wakati mzuri

London, England. Kiungo Paul Pogba ni miongoni mwa wachezaji wa Manchester United wanaotarajiwa kuwekwa sokoni mwisho wa msimu huu.

Kocha wa Man United, Jose Mourinho ametoa kibali cha mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuondoka.

Nyota wengine wanaotarajiwa kufunguliwa mlango ni Anthony Martial, Delay Blind na Matteo Darmian.

Mourinho amekuwa akitoa kauli tofauti kuhusu kiwango cha kupanda na kushuka cha Pogba tangu alipotua Man United kwa bei ghali.

Pogba ameibua mjadala upya, baada ya kucheza chini ya kiwango katika mchezo walionyukwa bao 1-0 na West Bromwich Albion.

Mourinho alimtoa kiungo huyo mshambuliaji na nafasi yake kujazwa na Mfaransa mwenzake Anthony Martial ambaye pia amekalia kuti kavu.