In Summary
  • Ingawa Serikali haijatangaza kuongeza masilahi ya watumishi, ripoti ya Benki Kuu inaonyesha mishara ya watumishi imeongezeka ndani ya miezi 12 iliyopita mpaka Oktoba 2018.

Ingawa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ina-onyesha ni watu 6,099 wame-ajiriwa ndani ya miaka mitatu iliyopita, ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania inaonyesha mishahara imeongezeka kwa takriban Sh31 bilioni kwa miezi 12 iliyopita.

Ripoti ya tathmini ya hali ya uchumi ya kila mwezi inayotole-wa na BoT inaonyesha Oktoba, Serikali ilitumia Sh553.3 bilioni kulipa mishahara ikiongezeka kutoka Sh522.4 bilioni zilizolip-wa Oktoba, 2017.

Ripoti hiyo ya Novemba inabainisha kuwa katika mwezi huo, Serikali ilikusanya Sh1.3 tri-lioni Oktoba huku ikitumia Sh1.5 trilioni. Katika kiasi kilichotumika ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 22.1, Sh893.4 bilioni zili-kuwa kwa matumizi ya kawaida na Sh635 zilitekeleza miradi ya maendeleo. Kati ya fedha za miradi, asilimia 72.6 zilikuwa mapato ya ndani.

Mishahara ya watumishi wa umma ilikuwa ni zaidi ya nusu ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida katika mwezi huo. Makadirio yanaonye-sha kuwa Sh553.3 bilioni ikiwa imepanda kutoka Sh522.4 bilio-ni zilizolipwa mwezi kama huo mwaka jana, sawa na ongezeko la Sh30.9 bilioni.

Mishahara hiyo imeongezeka katika kipindi ambacho katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi anasema ajira zilizotolewa ndani ya miaka mitatu iliyopita zilikuwa sawa na asilimia moja ya walioomba.Katika kipindi hicho, anasema walitangaza nafasi 6,554, lakini walipokea maombi kutoka kwa watu 594,300 na wakatoa ajira 6,099.

Kupata ufafanuzi wa ongeze-ko hilo, Mwananchi lilimtafuta Gavana wa BoT, Profesa Florens Luoga ambaye alisema yupo kwenye mkutano na akataka atu-miwe ujumbe mfupi wa maneno.Baada ya kumtumia maswali, Profesa Luoga alijibu: “Asante.

Utapigiwa simu na naibu gavana wa uchumi, fedha na mipango.”Baada ya muda, ofisa wa ofisi ya naibu gavana alipiga na kuse-ma ongezeko la mishahara ya watumishi limetokana na ajira mpya zilizotolewa pamoja na maboresho ya masilahi yaliyo-fanywa ndani ya kipindi hicho.“Kujua ni ajira kiasi gani zime-tolewa na mishahara ipi ime-pandishwa, wasiliana na mam-laka husika,” alisema ofisa huyo.

Mtalaamu wa masuala ya utu-mishi wa umma, James Ntobi anasema zipo sababu nyingi zin-azoweza kusababisha mishahara ya umma kupanda hata kama hakuna watu wengi walioajiriwa.

Anasema kwa kuangalia mazingira ya sasa: “Kuna watu wengi wamesimamishwa kazi kwa tuhuma mbalimbali kisha kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Hawa bado wanalipwa kama ilivyo kwa waliorithi nafasi zao. Hapa lazima mishahara iongezeke.”

Mauzo nje

Sio mishahara pekee iliyoongezeka, ripoti inaonyesha mauzo ya mazao ya biashara nje ya nchi na mapato yatokanayo na huduma hasa za usafirishaji na utalii yaliongezeka pia ndani ya kipindi hicho.

Licha ya mgomo wa wanunuzi uliojitokeza msimu huu wa mavuno, mauzo ya korosho nje ya nchi yaliongezeka kwa Dola 235.5 milioni (zaidi ya Sh541.6 bilioni).

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mauzo ya korosho yameimarika na kuiingizia Tanzania jumla ya Dola 575.6 milioni (zaidi ya Sh1.3 trilioni) ikilinganishwa na Dola 340.1 milioni (zaidi ya Sh782.2 bilioni) zilizopatikana mwaka ulioishia Oktoba 2017.

Takwimu hizo, ripoti inasema zimekusanywa kutoka vyanzo vya Mamlaka ya Mapato (TRA) na BoT. alipotafutwa meneja wa elimu kwa mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo ili kupata ufafanuzi juu ya ongezeko alisema wenye taarifa sahihi ni Bodi ya Korosho.

“Bodi ya Korosho watakupa taarifa sahihi zaidi. Watafute wao,” alisema Kayombo.

Mwanzoni mwa msimu wa mauzo ya korosho mwaka huu, wakulima waligoma kuuza mavuno yao kwa bei ndogo ambayo wanunuzi walikuwa tayari hata kuishawishi Serikali kutoa bei elekezi ya walau Sh3,000 kwa kilo.

Kutokana na hilo, ikawa zamu ya wanunuzi kugoma wakisema bei hiyo haitowalipa hivyo Serikali ikaamua kununua yenyewe ikilipa Sh3,300 kwa kilo.

Licha ya uamuzi huo, Rais John Magufuli aliiuvunja uongozi wa Bodi ya Korosho kutokana na kushindwa kuratibu vyema biashara ya zao hilo kwa manufaa ya mkulima na Serikali pia.

Hata hivyo, ufafanuzi wa ofisi ya naibu gavana unasema: “Mauzo hayo ni kwa miezi 12 iliyopita hivyo yanajumuisha msimu wa mwaka jana pia.”

Kwa ujumla, uuzaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi, uliongezeka hadi Dola 8.7 bilioni kutoka Dola 8.6 bilioni za Oktoba 2017. Ongezeko hilo lilitokana na kuimarika kwa mauzo ya mazao ya biashara yaliyoongezeka kwa asilimia 38.4.

Utalii na usafirishaji

Wakati akiba ya fedha za kigeni ikifika Dola 5.2 bilioni zinazotosha kununua huduma na bidhaa kwa miezi 5.2 na deni la Taifa likipanda hadi Sh62 trilioni, ripoti inaonyesha maboresho yaliyofanywa katika Bandari ya Dar es Salaam yaliongeza ufanisi hivyo mapato.

Maboresho hayo yaliongeza mzigo wa nchi zinazohudumiwa na bandari hiyo hasa Zambia, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.

Kuondolewa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye huduma za usafiri na usafirishaji, kuliongeza mapato ya sekta hiyo kwa asilimia 10.9 na kufika Dola 1.2 bilioni.

Sambamba na usafirishaji wa mizigo, ongezeko la watalii lilishamirisha mapato pia ambayo yalikua kwa asilimia 7.3 na kufika Dola 7.8 milioni ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita.