In Summary
  • Akiwasilisha mada kuhusu utambuzi, ofisa kilimo, Sergea Mutahiwa alisema mtazamo wa jamii na uelewa mdogo ni tatizo kuhusu viuatilifu vinavyopendekezwa na namna ya kutumia dawa za kuangamiza wadudu hao.

Kiteto. Wataalamu wa kilimo kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (Fao), wamewajengea uwezo wakulima wilayani hapa mkoani Manyara kuhusu namna ya kupambana na viwavijeshi vamizi.

Akiwasilisha mada kuhusu utambuzi, ofisa kilimo, Sergea Mutahiwa alisema mtazamo wa jamii na uelewa mdogo ni tatizo kuhusu viuatilifu vinavyopendekezwa na namna ya kutumia dawa za kuangamiza wadudu hao.

Mutahiwa alisema matumizi yasiyo sahihi ya viuatilifu yanaweza kusababisha kuua wadudu wasiolengwa na kudhuru afya za binadamu, vilevile kujenga usugu kwa visumbufu vya mimea.

Ofisa kilimo, Grace David alisema ukaguzi ni muhimu kubaini uwapo na kiwango cha viwavijeshi vamizi, kufanya tathmini ya madhara na kujua njia sahihi ya kudhibiti.