In Summary
  • Nguli huyo  kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametua na Ndege ya Shirika  la Kenya (Kenya Airways) akitokea Kinshansa na yuko tayari kwa kukonga nyoyo za mashabiki wake.

Mwanamuziki  Ngiama Makanda  maarufu kama Werason ametua nchini  saa tisa usiku wa kuamkia leo Aprili 8 huku mashabiki wakionywa kutotumia tiketi feki.

Nguli huyo  kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametua na Ndege ya Shirika  la Kenya (Kenya Airways) akitokea Kinshansa na yuko tayari kwa kukonga nyoyo za mashabiki wake.

Akizungumza na  gazeti hili  katika uwanja wa ndege, mmoja wa waratibu wa shoo hiyo, Yale Ngoss  V.I.P amesema mashabiki waliokuwa wanamsubiri Werrason wataambiwa lini atafanya shoo yake hapa nchini baada ya awali kuahirishwa.

Aidha mratibu huyo amesema  watu waliokata tiketi kwa mara ya kwanza watazitumia kwenye shoo itakayopangwa, ila wasifanye ujanja  wa kutafuta  tiketi feki.

 “Kwanza tunashukuru kwa ujio wake Werrason, na pia baadaye tutakaa tupange shoo ifanyike lini maana tulikuwa tunasubiri afike kwanza ndio tupange tarehe, yaani hapa  tunaanza upya, ila kwa wale wenye tiketi walizokata mara ya kwanza watazitumia hizohizo’’amesema

Werrason amekuja na wanamuziki wake 10 na wengine 14 wataingia leo,jumla wanatakiwa wawe ishirini na nne.