Element Club

Wapi- Masaki jijini Dar es Salaam

Jumamosi hii, DJ Sinyorita atakuwa anawarusha kwa muziki mtamu kuanzia saa tatu.

Kisasa Complex

 Wapi- Dodoma

Kama upo Dodoma wikiendi hii unaweza kupunguza uchovu wa kazi wa wiki nzima kwa kujirusha Kisasa Complex Club kuanzia leo Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

 

Serena Hotel Dar

Pata Iftar kila siku katika mwezi wa Ramadhani kuanzia Mei 16- Juni 17, 2018 ndani ya mgahawa wa Serengeti kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2.00 usiku.

 

Ambassador

Kama upo ndani ya Mji wa Geita  kiwanja hiki kipo katika barabara ya kuelekea mgodi mkubwa wa dhahabu. Ukiwa kwenye Club ya Ambassador utapata chakula kizuri,mchemsho wa ndizi samaki fresh na kuku.

 

Club 7

Kama upo katika makao makuu ya nchi, unaweza kujirusha Club 7 kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Mbali na muziki, chakula kizuri ni moja ya sifa inayoitofautisha Club hiyo na nyingine katika Jiji la Dodoma.