In Summary
  • P.Funky na Kajala wamezaa mtoto ambaye anaitwa Paula

Dar es Salaam: Baada ya kuwepo kwa tetesi za kurudiana kwa Msanii wa Filamu, Kajala Masanja na mtayarishaji wa muziki, P-Funk Majani, wenyewe wamekanusha.

Akizungumza na MCL Digital, Kajala amesisitiza kuwa kuwepo kwa ukaribu kati yao ni kwa ajili ya mapenzi kwa mtoto wao lakini hakuna kitu kingine kinachoendelea.

“Wakati ambao tulikuwa hatuonekani pamoja, tumegundua tulikuwa tunamnyima haki mtoto wetu ambaye kwa kipindi hiki anapotuona tupo karibu anafurahi,”amesema Kajala.

Ameongeza na kusema, katika ukaribu wao ni pale wanapokuwa wanakwenda shuleni kwa mtoto wao kwa pamoja kwa ajili ya kumtembelea.

Alipoulizwa kuhusu kusambaratisha ndoa ya P-Funk kutokana na ukaribu wao huo, Kajala amesema hakuna kitu kama hicho kwani mpaka leo mtayarishaji huyo yupo na mkewe nyumbani.