In Summary

Juni 9 mwaka huu meli ya MV Liemba inayofanya safari katika Ziwa Tanganyika itatimiza miaka 105 tangu ianze kufanya kazi. Meli hiyo iliyopachikwa jina la The African Queen ilianza kazi Juni 9, 1915 ikiwa chini ya Wajerumani ikifahamika kwa jina la Graf von Goetzen. Ndiyo meli kongwe zaidi ambayo inaendelea kufanya kazi ingawa katika vipindi tofauti imefanyiwa marekebisho.

Mv Liemba a.k.a The African Queen ndiyo meli kongwe duniani inayoendelea na kazi.

Juni 9 mwaka huu meli ya MV Liemba inayofanya safari katika Ziwa Tanganyika itatimiza miaka 105 tangu ianze kufanya kazi. Meli hiyo iliyopachikwa jina la The African Queen ilianza kazi Juni 9, 1915 ikiwa chini ya Wajerumani ikifahamika kwa jina la Graf von Goetzen. Ndiyo meli kongwe zaidi ambayo inaendelea kufanya kazi ingawa katika vipindi tofauti imefanyiwa marekebisho.

Kuingia Afrika Mashariki

Mv Liemba kabla ya mwaka 1916 iliitwa Graf Goetzen jina lilitokana na muundaji wa meli hiyo. Inalezwa kuwa iliingizwa nchini kutoka Ujerumani ikiwa vipuri katika makasha 5,000 yaliyobebwa na meli tatu za mizigo. Baada ya kufika Bandari ya Dar es Salaam yalisafirishwa kwa njia ya reli ya kati kuelekea Kigoma.

Kuzama kwa miaka 8

Zipo taarifa katika mtandao wa Warwick wa Ujerumani zinazosema kwamba meli ya MV Liemba katika vita ya kwanza ya dunia ilipigwa na kuzama kabla ya kuibuliwa miaka minane baadaye. Inaelezwa kuwa katika vita hiyo dhidi ya Waingereza Januari 15, 1916 ilipigwa na kuzama.

Meli hiyo ilibaki chini ya maji mpaka ilipokuja kuibuliwa 1924 na kupatikana ikiwa katika hali nzuri ambayo ilihitaji marekebisho kiasi ili irudi kazini.

Kusafirisha wakimbizi 75,000

Moja ya kazi kubwa ya kihistoria ambayo meli hii imewahi kufanya ni kuisafirisha wakimbizi 75,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1997.