In Summary
  • Akizungumza kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya Tapsea, Mwenyekiti Tapsea, Zuhura Maganga alisema chama hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji ikiwamo kufanya kazi katika muundo usiozingatia mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Chama Makatibu Mahsusi Tanzania (Tapsea) kimelalamikia masilahi duni ya kada hiyo ikiwamo mishahara midogo isiyolingana na majukumu ya utendaji kazi.

Akizungumza kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya Tapsea, Mwenyekiti Tapsea, Zuhura Maganga alisema chama hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji ikiwamo kufanya kazi katika muundo usiozingatia mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Alisema muundo huo hautoi fursa ya kupanda madaraja au vyeo kwa watumishi waliosoma na kupata sifa stahiki.

“Changamoto ya masilahi duni, mishahara midogo, baadhi ya waajiri kutotambua na kuzingatia mafunzo yanayotolewa na vyuo vinavyotambulika kama vigezo vya msingi vya kupanda madaraja, yamekuwa malalamiko yetu kwa muda mrefu,” alisema.

Alisema maadhimisho ya miaka 10 ya Tapsea alisema yatafanyika Zanzibar Mei 10 hadi 12 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu (Suza).

Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa wa Tapsea, Aneth Charles aliwataka makatibu mahsusi kufanya kazi kwa bidii ili kujenga uaminifu kwa waajiri wao.