In Summary
  • Kaimu meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya, Davis Mongate alisema mfanyabiashara anayefanya shughuli zake katika maeneo ambayo ni rasmi anatakiwa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Kutoogopa kwa wafanyabiashara kwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutasaidia kujenga ukaribu wa kupata ufafanuzi wa masuala yanayohusu kodi.

Msimamizi wa wiki ya elimu kwa mlipakodi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Tubagile Namwenje alisema juzi mjini hapa kuwa, pande hizo hazipaswi kuogopana kwa kuwa zinajenga nchi moja. “Inatakiwa walipa kodi watambue kwamba watumishi wa TRA ni maofisa wa Serikali na hakuna haja ya kuwaogopa kwa kuwa ni watu wanaoisaidia nchi yetu isonge mbele na sisi sote tunataka nchi hii ipige hatua kimaendeleo,” alisema.

Kaimu meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya, Davis Mongate alisema mfanyabiashara anayefanya shughuli zake katika maeneo ambayo ni rasmi anatakiwa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Mfanyabiashara Ester Ipembe alisema anafurahishwa na huduma anayoipata kutoka kwa maofisa hao na kuomba wafanyabiashara wenzake kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata elimu ya kodi.