Manjano (Turmeric) ni kiungo cha jamii ya mizizi.

Yana faida nyingi sana katika ulimwengu wa tiba kutokana na kutibu maradhi mbalimbali.

Ndiyo maana Wahindi huitia kwenye aina mbalimbali za vyakula.

Wataalamu waliobobea kwenye fani ya tiba mbadala wanasema, ikiwa utaichemsha manjano kwa dakika 15 kwenye maziwa halisi, inakuwa sawa na antibiotics.

Mchanganyiko huo unaleta nguvu ya kutibu maradhi mbalimbali kama figo kushindwa kufanya kazi.

Figo ni tatizo linaloweza kutibika kwa kutumia maziwa na manjano.

Kufeli kwa figo husababishwa na mambo mengi sana, baadhi yake ni kubana mkojo kwa muda mrefu, kutokunywa maji ya kutosha na kutumia chumvi nyingi.

Baadhi ya visababishi vingine ambavyo vinaepukika ni kula nyama mara nyingi zaidi, kutokula chakula cha kutosha, kuchelewa kujitibu maambukizi madogo madogo na kutumia dawa za maumivu bila maelekezo.

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke ni tatizo linaloweza kutibika kwa kutumia maziwa na manjano.

Tatizo hili hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke.

Uvimbe huu unajulikana kwa jina la ‘Ovarian Cyst.’

Hutokea kwa wanawake wa umri wowote na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito.

Tatizo hili linaweza kutibika kwa kunywa manjano yaliyochemshwa kwenye maziwa.

Kukosa choo

Mchemsho wa maziwa na manjano unatibu tatizo la kukosa choo. Kitaalamu kukosa choo kwa siku moja, siyo tatizo, isipokuwa mtu anaweza kutajwa kuwa na tatizo hilo iwapo atakosa choo zaidi ya saa 72, yaani siku tatu.

Ni vizuri binadamu akipata choo mara tatu ndani ya saa 24.

Waswahili husema ‘raha ya nyumba ni choo’ kwa hakika, hawakukosea kwa kuwa chakula chochote kinapoliwa lazima kitumike mwilini na mabaki yake hutolewa kwa njia ya haja kubwa.

Ugumu wa kuitoa haja kubwa husababisha maumivu makali na pengine kuzalisha maradhi mengine kama bawasili, kuumwa kichwa na homa.

Tatizo la kutopata choo linatokana na haja kubwa kwenda taratibu hivyo kuchelewa kutoka kwa wakati mwafaka.

Dalili za kuwa na tatizo ni mgonjwa kupata maumivu ya tumbo ambayo hutokana na tumbo kujaa gesi.

Mtu mwenye tatizo la kukosa choo mara nyingi tumbo lake huvimba na kujaa gesi muda wote, hali hii inatokana na kuwa na uchafu tumboni.

Mwenye tatizo hili anywe manjano yaliyochemshwa kwenye maziwa.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa tiba mbadala