In Summary

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema leo Ijumaa Januari 11, 2019 watuhumiwa 12 wanaodaiwa kusafirisha shehena ya dhahabu kutoka Mwanza kwenda Geita watafikishwa mahakamani, kusomewa mashtaka yanayowakabili

 


Mwanza. Watu 12 wakiwemo askari polisi wanane watapandishwa kizimbani muda wowote leo Ijumaa Januari 11, 2019 katika mahakama ya hakimu mkazi Mwanza.

Wamefikishwa mahakamani hapo leo na wanasubiri kupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Watu hao wanadaiwa kuhusika na tukio la kusafirisha shehena ya dhahabu kilo 323.6  na  fedha taslimu Sh305 milioni kutoka mkoani Mwanza kuelekea Geita.

Wanashikiliwa na polisi tangu tukio hilo lilipotokea Januari 5, 2019.

Askari watakaopandishwa kizimbani leo walitajw ana Rais John Magufuli siku mbili zilizopita kuwa wanadaiwa kuhusika katika tukio hilo, kuwasaidia wahusika kufanikisha kusafirisha shehena hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi