In Summary

Waandishi wa habari, wapo katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salam ambapo mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ametekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya leo.


Dar es Salaam. Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wameweka kambi nje ya Hotel ya Colosseum alipotekwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ kujua kinachoendelea.

Ndani ya uzio wa hoteli hiyo iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam kuna gari ya polisi ya kutoka wilaya ya Kinondoni pamoja na gari aliyoingia nayo ‘MO Dewji’ likiwa bado limeegeshwa eneo la tukio.

Upande wa pili wa jengo hilo kuna hoteli ambapo shughuli zinaendelea kama kawaida wakati jengo linalotumika kwa GYM likiwa haliruhusiwi mtu yeyote kuingia huku askari waliovaa kiraia wakizunguka eneo la tukio.