In Summary

Walioripoti leo ni wawili tu, Dk Vicent Mashinji na Salum Mwalimu


Dar es Salaam. Viongozi wa Chadema waliotakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi leo Jumanne Machi 13, 2018 wametakiwa kufika tena kituoni hapo Machi 16, 2018.

Licha ya kutakiwa kuripoti viongozi saba, waliofanikiwa kufika kituoni hapo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji na naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu.

Viongozi wengine watano akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wameshindwa kuripoti kutokana na kuhudhuria vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vilivyoanza leo mjini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo, wametakiwa kuripoti Machi 16, saa 2:00 asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho Dk Mashinji amesema, “Viongozi wote wameshatoa maelezo yao. Leo tumeripoti wawili na viongozi wengine ni wabunge na wapo Dodoma walishindwa kujigawa katika mambo mawili.”