In Summary

Katika gari hilo walikuwemo vijana 210 waliokuwa wanakwenda Mbeya kwa ajili ya mafunzo ya vitendo 

Mbeya. Zaidi ya Vijana 10 waliokuwa wakielekea kwenye mafunzo ya vitendo katika kambi ya JKT ItendeMbeya, wahofiwa kufariki dunia baada ya basi walilopanda kupata ajali eneo la mteremko wa Igodima, nje kidogo ya mji wa Mbeya.

Akizungumza na MCL Digital leo Juni 14, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Musa Talibu amesema vijana hao walikuwa wakitokea kambi ya Igunga Mkoani Tabora  wakielekea kambi ya mafunzo ya jeshi ya Itende, Mbeya.

Kamanda Taibu alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha gari kwa kasi bila kufuata alama za barabarani.

“Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva ambae pia ni mmoja ya waliofariki papo hapo, vijana hawa wametokea Mkoani Tabora walikuwa wanakuja Mbeya kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika kambi yetu ya Itende. Mpaka sasa hatuna tarifa kamili za idadi ya majeruhi”, alisema Taibu.

 Kamanda huyo alisema, katika gari hilo walikuwemo vijana 210 waliokuwa wanakwenda Mbeya kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika kambi ya Itende.