In Summary

Ashangaa kusikia amewekewa matanga nyumbani kwake


Rapa wa bendi ya FM Academia, Hitler Norma Benga ‘Hitler’ ambaye taarifa za kifo chake zilianza kuzagaa asubuhi ya leo Juni 13, ameibuka na kusema aliyefariki ni dereva wa bodaboda aliyokuwa amepanda.

Leo asubuhi zilikuwapo taarifa kwamba mwanamuziki huyo amefariki kwa ajali ya pikipiki akiwa Kibaha, mkoani Pwani.

Amesema taarifa zilizagaa kuwa amefariki baada ya kupata taarifa kutoka katika simu yake ambayo aliipoteza katika eneo la tukio.

“Aliyeiiba simu yangu naona alijua ni ya dereva aliyefariki akaanza kuwapigia watu wangu wa karibu kuwa mwenye simu amefariki,” anasema Hitler.

Amesema alishangazwa kusikia watu wakizungumzia taarifa za kifo chake baada ya marafiki zake kukusanyika nyumbani kwake Mwananyamala Kwa Kopa, jijini Dar es Salaam.

Awali kiongozi Msaidizi wa Bendi ya FM Academia, Christian Mene, amezungumza na MCL Digital na kusema kuwa Hilter ni mzima na wala hahusiki na ajali hiyo.

“Kwanza tunawapa pole ndugu zetu wote waliopata usumbufu wa taarifa hizi za Hitler kuwa amefariki, ukweli ni kwamba hajafariki,” anasema