In Summary

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla na nafasi yake kumpangia Juma Homera aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.

Dar es Salaam. Jana Rais John Magufuli alimteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuchukua nafasi ya Amos Makalla aliyekuwa mkuu wa mkoa huo.

Kuondolewa kwa Makalla katika nafasi hiyo kunaweza kuwa kumesababisha na baadhi ya mambo ambayo Rais Magufuli aliwahi kuyasema katika mikutano yake ya hadhara akiwa mikoani.

Moja ya mambo hayo ni kwamba atampatia cheo Homera kama kuna mkuu wa mkoa anayelegalega