In Summary
  • Chama kinachoondoka madarakani kimetuma ujumbe wa pongezi kwa mshindani wake huku asilimia 99 ya kura zikiwa tayari zimehesabiwa

Oslo, Finland. Wakati kura zikiendelea kuhesabiwa katika matokeo ya ubunge nchini Finland, Chama cha Social Democratic cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto, kinaelekea kupata ushindi

Matokeo hayo yanampatia kiongozi wa chama hicho, Antti Rinne aliyewahi kuwa waziri wa fedha jukumu la kutafuta washirika wa kuunda Serikali ya Muungano.

Chama hicho kilipata uungwaji mkono wa asilimia 17.7 baada ya kufanya kampeni ya kupinga hatua za kubana matumizi zilizoanzishwa na Serikali inayoondoka madarakani ya siasa za wastani za mrengo wa kulia.

Waziri Mkuu, Juha Sipila ametuma salamu za pongezi kwa upinzani baada ya chama chake kushindwa katika uchaguzi. Finland inapanga kuchukua urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya mwezi Julai.