In Summary

Amefafanua hatua hiyo inatarajiwa kuongeza ajira na mapato ya Serikali.


Dodoma. Serikali imependekeza kuongeza asilimia 10 kwenye ushuru wa forodha kwenye unga wa gypsum kwa mwaka mmoja.

Hayo yamesemwa leo Juni 14 na Waziri wa Fedha Phillip Mpango bungeni mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka 2018/19.

Amesema marekebisho haya yanalenga  kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo hapa nchini na kuhamasisha wawekezaji watumie "gypsum' inayopatikana hapa nchini ili kuzalisha "gypsum" powder.

Amefafanua hatua hiyo inatarajiwa kuongeza ajira na mapato ya Serikali.