In Summary

Masogange alifariki dunia Ijumaa Aprili 20, 2018


Mbeya. Baadhi ya wasanii wamewasili nyumbani kwa wazazi wa marehemu Agnes Gerald (Masogange), Mbalizi II wilayani Mbeya, ambako mazishi yatafanyika leo Aprili 23, 2018.

Msanii Zuwena Mohamed (Shilole) yupo msibani akishirikiana na waombolezaji wengine kuandaa chakula.

Mbali ya kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na Bongo Movie, Shilole anamiliki mgahawa uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Masogange aliyefariki dunia Ijumaa Aprili 20, 2018 katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam anazikwa leo Aprili 23, 2018.