Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema licha ya uchumi kuwa imara lakini thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani ilishuka kidogo.

Akizungumza leo Juni 13, wakati akiwasilisha mwenendo wa uchumi kwa mwaka 2017, Dk Mpango amesema thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ilikuwa ya kuridhisha ikibadilishwa kwa Sh2, 228 kwa dola moja.

"Hadi Desemba mwaka 2016 Dola moja ilikuwa inabadilishwa kwa Sh2, 177 na mpaka Desemba 2017 kulikuwa na tofauti ya wastani wa Sh57.79," amesema Mpango.

Mwenendo huo, amesema umetokana na kuboresha kwa usimamizi, utekelezaji wa Sera thabiti za bajeti na fedha na mwenendo mzuri wa urari wa mapato ya fedha za kigeni.