In Summary
  • Naibu Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Subira Mgalu amesema hajaridhishwa na kasi ya kampuni ya Urban and Rural Engineering Service aliyepewa tenda ya kusambaza umeme katika Wilaya ya Kibondo na Kakonko mkoani Kigoma.

Kibondo. Naibu Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Subira Mgalu amesema hajaridhishwa na kasi ya kampuni ya Urban and Rural Engineering Service aliyepewa tenda ya kusambaza umeme katika Wilaya ya Kibondo na Kakonko mkoani Kigoma.

Akizungumza leo Alhamisi Julai 11, 2019 na wakazi wa kijiji cha Nyange kata ya Mabamba katika uzinduzi wa umeme katika zahanati ya kijiji hicho, Subira amesema amesema kama mkandarasi huyo ataendelea na kasi hiyo Serikali itamchukulia hatua.

Amesema Kibondo mpaka sasa ni vijiji 3 kati ya 40 vyenye umeme huku Kakonko kukiwa na vijiji vitano kati ya 29, akibainisha kuwa hadi Juni 2020 vijiji vyote vinatakiwa kuwaka umeme.