In Summary

Swala ya Idd kitaifa itafanyika jijini Dar es Salaam kutegemea muandamo wa mwezi.

 


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limejipanga kuimarisha ulinzi maeneo yote ya fukwe na starehe wakati wa Sikukuu ya Idd El Fitri.

Akizungumza na wanahabari leo, Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watatumia helikopta, farasi, bodaboda na magari kuimarisha ulinzi.

"Katika mikoa yote mitatu ya kipolisi tumejipanga kuimarisha ulinzi kwa kutumia helikopta, farasi, pikipiki na magari, " amesema.

Swala ya Idd kitaifa itafanyika jijini Dar es Salaam kutegemea muandamo wa mwezi.