In Summary

Kampuni ya ndege ya Emirates imetambulisha mlo mpya (menu) kwa abiria wake wanaosafiri kutoka Afrika Mashariki kuelekea Dubai.


Kampuni ya ndege ya Emirates imetambulisha mlo mpya (menu) kwa abiria wake wanaosafiri kutoka Afrika Mashariki kuelekea Dubai.

Meneja usimamizi wa vyakula wa kampuni hiyo kanda ya Afrika, Nasser Iskeirjah katika taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vy a habari imeeleza kuwa abiria wanaosafiri kutoka Dar es Salaam, Nairobi na Addis Ababa watapata mlo mpya ambao ni wa Kiafrika zaidi.

Alisema wapishi wao walifanya utafiti kwa kuwahoji wateja wao muda mrefu kabla ya kuja na aina mpya ya vyakula katika ndege zao.

Kila chakula kitakachopatika katika ndege hizo kutokea Afrika Mashariki kitakuwa na asili ya eneo hilo akitolea mfano mchuzi wa nani na kuku wa kupaka.

“Lengo letu ni kutoa chakula kizuri kwa wateja wetu wawapo angani nasi, kuanzia burudani na vyakula,” alifafanua.

Kati ya mwaka 2017 na 2018 shirika hilo limesafirisha abiria zaidi ya milioni moja kutoka Nairobi, Dar es Salaam na Addis Ababa.