In Summary
  • Mpango ulioanzishwa una lengo la kuwahamasisha wanafunzi kutambua mapema taaluma zao

Dar es Salaam.  Vijana wenye matumaini ya kufanya kazi benki huenda wakapewa nafasi kubwa ya kupata kazi baada ya Benki ya NIC kuanzisha mchakato wa mafunzo.

Benki hiyo imeanza kufundisha wanafunzi wa shule za sekondari mambo mbalimbali ya kibenki.

Mkurugenzi Mkuu wa NIC, Mick Karima alisema jana Jumatatu Aprili 1, 2019 kuwa lengo ni kuhamasisha wanafunzi kutambua mapema taaluma zao na kuchagua wanataka kufanya kazi gani pindi wanapomaliza masomo.

 “Mara nyingi wanafunzi wanasoma bila kujua au kuchagua kazi gani wanayoitaka kufanya. Wakitembelea sehemu kama hii, wakikutana na watu waliowatangulia na kuelezwa mambo mbalimbali yakiwemo ya kibenki inawasaidia kuchagua wanachotaka,” amesema.

Karima alishauri wanafunzi kuhakikisha wanawasikiliza viongozi wanapozungumza mambo mbalimbali yanayoikabili nchi ili wakikua waweze kutatua changamoto.