In Summary

Mzee Thomas Markle ameuambia mtandao wa Marekani wa TMZ Jumatano kuwa hataweza kuhudhuria katikati ya mzozo wa picha zilizotolewa na paparazzi akisema atahudhuria; mara hatahudhuria kutokana na operesheni ya moyo anayotarajia kufanyiwa.


London, Uingereza. Wasiwasi umetanda kuhusu uwezekano wa baba mzazi wa bi harusi mtarajiwa Meghan Markle kuwepo kushuhudia ndoa ya binti yake huyo atakapokuwa anaolewa na Prince Harry Jumamosi.

Mzee Thomas Markle ameuambia mtandao wa Marekani wa TMZ Jumatano kuwa hataweza kuhudhuria katikati ya mzozo wa picha zilizotolewa na paparazzi akisema atahudhuria; mara hatahudhuria kutokana na operesheni ya moyo anayotarajia kufanyiwa.

Dada wa kambo wa Markle, amesema anakabiliwa na “msongo wa mawazo usio wa kawaida".

Akizungumza katika kipindi cha TV cha Good morning Britain kutoka Orlando, Florida, dada huyo Samantha Markle alisema hakuwa na uhakika ikiwa Markle atasafiri kwenda Windsor.

"Alinitumia ujumbe kwamba atafanyiwa operesheni ya moyo,” alisema. "Sote tunatumaini atapita salama katika hili."

Wakati huo huo, makazi ya Kensington yametangaza kwamba Princess Charlotte atakuwa miongoni mwa wapambe wa harusi na ndugu yake Prince George ataongoza harusi hiyo mwishoni mwa juma.

Markle alikumbwa katika matukio tata mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya ripoti kwamba alipigwa picha na paparazzi akionekana anafanya maandalizi ya harusi hiyo.

Picha hizo zilimwonyesha Markle – akiwa hafahamu lolote kama anapigwa picha – akiwa katika matukio mfululizo yenye uhusiano na harusi, ikiwemo ya kupima suti ya harusi.

Jumatatu Markle aliripotiwa akiuambia mtandao wa TMZ kwamba hatahudhuria harusi hiyo. Mtandao huo uliripoti kwamba Markle alikuwa anataka kuhudhuria lakini huenda akashindwa kutokana na tatizo la afya.

Ripoti ya tatu ya mtandao huo ilisema masuala ya afya na operesheni iliyopangwa vitamzuia kuhudhuria.